Hii blog ni kwa ajili ya kuitikia mwaliko wa Mtaguso wa pili wa Vatikano wa kuwafanya wakatoliki wote waifahamu liturjia takatifu wanayoiadhimisha. Nitatoa utafiti wangu juu ya liturjia na nitakuwa tayari kujibu maswali yenu juu ya liturjia. Karibuni sana!The aim of this blog is to impart liturgical knowledge to the people of God. It targets mainly the people from the swahili speaking countries. Welcome for the sharing of knowledge about our liturgy!
July 7 2010
Wapendwa katika Kristu,
Nawakaribisha kwa moyo mkunjufu katika blog hii inayozungumzia mambo ya liturjia. Nitajitahidi sana kila siku kuweka jambo jipya linaelimisha na kufunza juu ya imani yetu na zaidi juu ya liturjia takatifu. Katika blog hii nitatumia zaidi lugha ya Kiswahili, Kihaya na Kiingereza. Nikipata habari njema katika lugha nyingine kutoka katika blog na tovuti nyingine nitaiweka pia. Kwani nakumbuka Mwalimu wetu mpendwa huko Seminari Kuu ya Kibosho, Marehemu Fr. Seenga (R.I.P), maarufu kama Prof. M, alituambia ukweli ambao nimeuishi katika siku za karibuni: "Kujua lugha moja ni kama kusimama kwa mguu mmoja". Basi nawaalika kujifunza, kwa wale wenye nafasi na muda, lugha nyingine ili mpanue wigo wenu katika dunia hii ya utandawazi. Mimi nami bado najifunzaKijerumani na Kifaransa. Ila hali yangu ya Kifaransa ni mbaya. Ninategemea pia kujifunza Kisukuma, Luganda na lugha nyingine za Kanda ya Ziwa, Mungu akipenda.
Nawatakia usomaji mzuri na karibuni sana katika blog hii.
G. Mutarubukwa