Overblog
Edit post Follow this blog Administration + Create my blog
liturjia-takatifu.over-blog.com's name

Hii blog ni kwa ajili ya kuitikia mwaliko wa Mtaguso wa pili wa Vatikano wa kuwafanya wakatoliki wote waifahamu liturjia takatifu wanayoiadhimisha. Nitatoa utafiti wangu juu ya liturjia na nitakuwa tayari kujibu maswali yenu juu ya liturjia. Karibuni sana!The aim of this blog is to impart liturgical knowledge to the people of God. It targets mainly the people from the swahili speaking countries. Welcome for the sharing of knowledge about our liturgy!

Elimu ya Mambo ya Kiliturjia

Masomo ya Liturjia: mwanafunzi au mtaalamu mambo ya Liturjia anafanya nini?

Mwanafunzi au mtaalamu wa mambo ya liturjia anatafuta kujua zaidi undani wa teolojia ya Liturjia, uhusiano wake na shughuli za kichungaji, chanzo, maendeleo na mabadiliko yake katika historia, sheria na taratibu zinaongoza Liturjia, na liturjia na maisha ya kiroho (Rejea Sacrosanctum Concilium 16). Teolojia ya Liturjia ni juhudi na bidii wafanyazo wakristu wa vizazi vyote kutafakari juu ya Ibada ya kumwabudu  na kumtukuza Mwenyezi Mungu na kutafuta uhusiano uliopo kati yake na imani na maisha ya kikristu.[1]

 

Basi kwa kuwa Liturjia na maisha ya Kikristu ni chanda na pete, mwanafunzi au mtaalamu wa Liturjia uzama zaidi kwenye historia ili kujua jinsi uadhimishaji wetu wa Fumbo la Pasaka (Kiini cha Liturjia),  ulivyokua na kujiweka vizuri katika maisha ya watu wa nyakati na mazingira mbalimbali. Mwanafunzi wa Liturjia atasoma historia ya Liturjia, Liturjia na Neno la Mungu, Teolojia ya Liturjia, Liturjia na Anthropolojia (Anthropology),  Liturjia na Maisha ya Kiroho, Liturjia na Uchungaji, Sala ya Kanisa, Liturjia za Makanisa ya Mashariki, Liturjia ya Kanisa la Milano Italia, Liturjia na Utamadunisho, Liturjia katika Maandishi ya Mababa wa Kanisa, Vitabu vya Liturjia, Maadhimisho ya Sakramenti na Visakramenti mbalimbali, Uchambuzi wa Maandiko ya Kiliturjia (Critical and Hermaneutical Interpretation of liturgical Texts), Mbinu za kufanya utafiti katika mambo ya Liturjia (Methodology), n.k. Orodha ni ndefu sana, kwa taarifa zaidi unaweza kusoma tovuti (kiitaliano)hii http://www.santanselmo.org/home.htm.

 

Sasa nadhani umeona ni mambo gani wanafanya wanaliturjia kwa upande wa masomo. Kwa upande wa maisha ya kikristu, kila mkristu ni mwanaliturjia kwa sababu kama nilivyosema inabidi kila mtu atafakari daima uhusiano uliopo kati ya liturjia, imani na maisha ya kila siku. Ndio maana mababa wa Kanisa wa mashariki wanasema: “Tunaishi kile tunachoadhisha” yaani “we live what we celebrate”. Ili kufanikiwa kufanya hayo yote niliyoeleza hapo juu ni muhimu kujua lugha za Kilatini, Kigiriki, Kiitaliano, Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani, Kispanyolo, na lugha nyingine za mashariki kama Kiebrania, Kisiria cha zamani n.k.

 

Hiyo ndiyo hali ya mwanafunzi wa Liturjia na mtaalamu wa liturjia. Kazi yao kubwa ni kutoa elimu ya mambo ya liturjia kwa jamii kama kuitikia mwaliko wa mtaguso wa pili wa Vatikano, ili waamini wafaidike zaidi na maadhimisho wayoshiriki kila mara katika maisha yao (Rejea Sacrosanctum Concilium 14-20). Mwanafunzi wa liturjia hajifunzi kama wengi wanavyofikiria, jinsi ya kutumikia Misa au ile miongozo iliyoandikwa kwa rangi nyekundu katika Misale ya wauminii maarufu kama Rubrics. Kujua hayo ni wajibu wa kila mkristu. Anapaswa kujua hayo kabla ya kwenda kwenye Chuo kinachotoa elimu ya Liturjia kama kile cha Mtakatifu Anselmo cha Roma, niliposoma.

 

Basi kwa kumalizia nadhani umekeleketwa kuwa mmoja wa wanaojifunza mambo ya Liturjia. Karibu sana katika uwanja juu unaovutia sana kwa sababu utajua mambo mengi hata zaidi ya Teolojia kwa sababu liturjia ni maisha ya watu wa nyakati mbalimbali, na maisha ni zaidi ya Teolojia...yana mambo mengi hata yale ya kijamii, kiuchumi, kisiasa n.k.

 

G. Mutarubukwa

 


[1] A. CATELLA, «Theology of the Liturgy », in Handbook of Liturgical Studies. Fundamental Liturgy 2, ed. A. J. Chupungco, Collegeville 1998,  21. In English it is as follows: The theology of liturgy is «the effort on the part of all Christian generations to reflect on the experience of worship and to grasp the relation between faith and praxis». But This description of the theology of Liturgy sounds better in Italian because of the verb «intercorrere» , which seems to diminish the sense transmitted in English. I shall give here the Italian version of this: La teologia della liturgia è «l’impegno da parte di tutte le generazioni cristiane di riflettere sulla esperienza del culto e di cogliere il rapporto che intercorre (deve intercorrere) tra la fede e la prassi celebrative…».

MATHAYO

Share this post
Repost0
To be informed of the latest articles, subscribe:
Comment on this post