Overblog
Edit post Follow this blog Administration + Create my blog
liturjia-takatifu.over-blog.com's name

Hii blog ni kwa ajili ya kuitikia mwaliko wa Mtaguso wa pili wa Vatikano wa kuwafanya wakatoliki wote waifahamu liturjia takatifu wanayoiadhimisha. Nitatoa utafiti wangu juu ya liturjia na nitakuwa tayari kujibu maswali yenu juu ya liturjia. Karibuni sana!The aim of this blog is to impart liturgical knowledge to the people of God. It targets mainly the people from the swahili speaking countries. Welcome for the sharing of knowledge about our liturgy!

Misa ya Kiafrika Ujerumani au "Die afrikanische Messe"

Natimiza ahadi yangu ya kukuletea habari juu ya Misa ya Kiafrika huko Ujerumani, ijulikanayo zaidi kama "Afrikanische Messe". Baada ya kusoma habari hii utaweza kujua kwa nini Misa hii inaitwa "Afrikanische".

Tarehe 1 Agosti 2010 tumeadhimisha Misa hapa Wolfenbuettel, katika kanisa la parokia la Mt. Petro. Kila kitu kilikuwa kama tulivyokuwa tumepanga, isipokuwa hali ya hewa haikuwa na joto la kuDSCF5617.jpgtosha kuchangamsha damu ipasavyo kama huko kwetu Afrika. Wazungu wengi ambao hawajui Afrika ya kweli, wanadhani kuwa Afrika ina joto la kuua mtu kama kwenye tanuru ya matofali au ya kuoka mikate. Hiyo ndiyo Afrika waonayoona kwenye Luninga na vyombo vingine vya habari.

Misa inaitwa ya kiafrika kwa kuwa tunaimba nyimbo za dini za kiafrika na tunatumia ngoma na zana nyingine za muziki za kiafrika. Basi Misa inachangamka na kuwa na hali kama ya Afrika. Waimbaji wanatoka Ulaya na Afrika, yaani wapo wazungu  wanaojua kuimba nyimbo za Kiswahili za dini. Nyimbo nyingine zilikuwa za Kijerumani. Sehemu muhimu za Misa zinabaki za Kijerumani na Misa inafuata mtiririko wa kawaida wa Misa kama ulivyo katika Misale ya Waumini. Misa inakuwa na sehemu mbili, Liturjia ya Neno na Liturjia ya Ekaristi Takatifu (Nitaandika juu ya sehemu za Misa siku nyingine).

Kitu cha pekee ambacho kimefanyika kisicho cha kawaida katika Misa ni kwamba kumekuwa na igizo fupi kabla ya mahubiri na pia tulitumia picha mbalimbali kuelewesha watu. Mambo haya hasa maigizo wakati wa ibada hayaendani vizuri na utaratibu wa wakatoliki wa kuadhimisha Ekaristi; lakini watu wa eneo hili la Ujerumani wamezoea kufanya hivyo.

Nadhani mpaka sasa utakuwa umeelewa kwa nini hii Misa hiyo inaitwa ya Kiafrika. Sababu ni nyimbo, ngoma, vigelegele, kupiga makofi, uchangamfu, vifijo, ndelemo na zaidi Padre mwafrika ambaye utasikia watu wanamuita "Schwarz". Huyu sio Schwarzenegger, bali ni kama mimi ninavyoonekana katika picha hapo juu. Watu wanapenda Misa hii na inaudhuriwa na watu wengi hata wasio wakatoliki. Baada ya Misa na mlo wa pamoja utasikia wakiuliza juu ya Misa kama hiyo mwaka ujao. Basi kama kawaida jibu ni "Mungu akipenda na kutujalia uhai".

Share this post
Repost0
To be informed of the latest articles, subscribe:
Comment on this post
D

nimependa "barua" hii. lakini, picha ni ndogo mno, kwa sababu siwezi kukiona kischwa yake jinsi inayofaa! nadhani sasa unaupanga mizigo wako ili urudi Tanzania.
tulirudi kutoka barahi juzi, na tutakwenda mlimani kesho. baadaye, tutarudi kazini! brrrrrh!
salamu kwa wote tanzania! je t'embrasse!

Reply
I

Asante sana Dominique kwa barua yako. Ni kweli sasa nafunga mizigo yangu kurudi Tanzania. Nakutakia likizo njema mlimani na kazi njema baadaye. Nadhani uliweza kuelewa vizuri kiswahili
changu.  Wasalimie wote nyumbani na La Fare. Je t'embrasse!