Overblog
Edit post Follow this blog Administration + Create my blog
liturjia-takatifu.over-blog.com's name

Hii blog ni kwa ajili ya kuitikia mwaliko wa Mtaguso wa pili wa Vatikano wa kuwafanya wakatoliki wote waifahamu liturjia takatifu wanayoiadhimisha. Nitatoa utafiti wangu juu ya liturjia na nitakuwa tayari kujibu maswali yenu juu ya liturjia. Karibuni sana!The aim of this blog is to impart liturgical knowledge to the people of God. It targets mainly the people from the swahili speaking countries. Welcome for the sharing of knowledge about our liturgy!

Mwaka wa Kanisa

liturgical_year1.jpgMwaka wa Kanisa[1] (Sehemu ya kwanza) 

Mwaka wa Kanisa ni maadhimisho ya Matendo makuu ya Ukombozi wetu katika kipindi cha mwaka mzima.[2] Mungu ametukomboa na utumwa wa dhambi kwa kumtuma Mwanae mpenzi Bwana wetu Yesu Kristu. Kristu ametukomboa kwa kukubali kuupokea Msalaba, yaani Mateso na Kifo na baada ya siku tatu Kufufuka. Kwa hiyo, kiini au mutima wa mwaka wa Kanisa ni Fumbo Kuu la Pasaka, Mateso, Kifo msalabani na Ufufuko wake Kristo. Mtaguso wa pili wa Vatikano katika sehemu inayohusu Liturjia, yaani kwa kilatini Sacrosanctum Concilium, unatufundisha kuwa katika mwaka mzima tunaadhimisha Fumbo la Kristu kuanzia Umwilisho wake hadi siku ya Pentekoste na matumaini ya kuja kwake mara ya pili (SC 102). Fumbo la Pasaka na adhimisho lake ni kiini cha Liturjia yetu iwe ya kila siku, kila juma na kila mwaka.[3]

Adhimisho la mwaka wa Kanisa ni ishara ya shukrani ya waumini kwa Mwenyezi Mungu aliyetupatia ulimwengu na vyote vilivyomo. Ametupatia zawadi ya muda ambao inabidi tuutumie kumtukuza, kumshukuru na kwa kufanya hivyo nasi tupate kubarikiwa na kujaliwa kila kitu tunachohitaji katika maisha ya hapa duniani na baadaye huko mbinguni. Mwaka wa Kanisa haupingani na mwaka wa kawaida. Mwaka wa Kanisa uanza mapema na Dominika ya kwanza ya Majilio. Hata hivyo mwaka wa Kanisa ni njia ambayo waumini huitumia kuadhimisha Fumbo la Pasaka katika mtililiko mzima wa mwaka wa kawaida.

 

Kristu alijifanya mtu na kuingia katika historia ya binadamu ili awakomboe watu wa nyakati zote. Jukumu la Kanisa ni kuwafanya watu wafahamu ukweli huu na kuwafikishia watu ukombozi huu wa Kristu. Kanisa linatimiza jukumu hilo kwa kutangaza Neno la Mungu, kuadhimisha sakramenti mbalimbali na katika shughuli zake mbalimbali za kichungaji.[4]

 

Kwa nini tunaadhimisha Fumbo la Kristu kila mwaka? Kanisa linaadhimisho Fumbo la Kristu mara kwa mara ili kutangaza kwanza ukombozi wetu uliopatikana kupitia fumbo hilo na pia ili kutufanya sisi waumini wa leo tushiriki kikamilifu leo na sasa katika fumbo hilo la Kristu.[5] Kwa maadhimisho ya Liturjia katika mwaka wa Kanisa tunaishi leo na sasa nguvu za Fumbo hilo la ukombozi wetu. Maadhimisho ya mwaka wa Kanisa tunaweza kuyalinganisha na kupanda mlima kwa kutumia barabara inayozunguka mlima huo mpaka kileleni. Na kilele cha mlima huo ni maisha ya milele huko mbinguni yaani utimilifu wa Ukombozi wetu katika Kristu. Kila mwaka tunazunguka mlima huo. Haturudi tulipokuwa bali tunapanda juu zaidi ya tulipokuwa katika maisha ya kikristu na utakatifu. Hivyo basi adhimisho la mwaka wa Kanisa linatufanya tukue katika ukristu wetu. Katika mwaka wa Kanisa tunaangalia tulipotoka, tulipo na tunapoelekea.

 

Mwaka wa Kanisa, kulingana na maelezo ya Adolf Adam, ni mkusanyiko wa kiliturjia wa sherehe, sikukuu, kumbukumbu na maadhimisho mbalimbali ya Kanisa uliopangwa vizuri katika mzungukuko mzima wa mwaka.[6] Basi imani ya Kanisa inaoneka na kuchukua umbo halisi katika mwaka mzima wa Kanisa.

lit_cycle.gif

 

Mwaka wa Kanisa umegawanywa katika vipindi vinne:[7] Majilio (rangi ya urujuani) na Noel (rangi nyeupe au dhahabu), Kipindi cha Majuma ya Mwaka (Kijani Kibichi), Kwarezima(rangi ya urujuani) na

Pasaka(rangi nyeupe au dhahabu). Hivyo basi kila mara unapokwenda kusali angalia vizuri rangi za mavazi ya Misa ya Padre na baadhi ya vitambaa vya Altare na Tabernakulo, kwa rangi yake utatambua ni kipindi gani cha mwaka wa Kanisa tunaadhimisha.  Rangi nyekundu ni kwa ajili ya Jumapili ya Matawi, Ijumaa Kuu, Pentekoste, na Sherehe au Sikukuuu au Kumbukumbu za watakatifu mashahidi waliomwaga damu yao kwa ajili ya imani yao. Katika mwaka wa Kanisa tunaadhimisha pia Sherehe na Sikukuu za Bwana, Sherehe, Sikukuu na Kumbukumbu za Watakatifu mbalimbali.

Itaendelea......

 


[1] Picha imetolewa hapa: http://www.google.de/imgres?imgurl=http://www.stephrem.org/pictures/liturgical_year.jpg&imgrefurl=http://www.stephrem.org/liturgical_year.htm&h=778&w=700&sz=190&tbnid=4eOgU3aE1w7hOM:&tbnh=142&tbnw=128&prev=/images%3Fq%3Dimage%2Bliturgical%2Byear&hl=de&usg=__aXAPyaZFhjIL--Ngnphi8MW0GO4=&sa=X&ei=spQ1TJijI4SsOPWR0asE&ved=0CDUQ9QEwBw

[2] Cf. A. Adam, The Liturgical Year: its History and its meaning after the reform of the Liturgy, Collegeville 1990, vii.

[3] Cf. Paul VI, Mysterii Paschalis: On Liturgical Year and New Universal Roman Calendar, Rome 14 February 1969

[4] Cf. A. Adam, The Liturgical Year, viii.

[5] Cf. A. Adam, The Liturgical Year, viii.

[6] Cf. A. Adam, The Liturgical Year, viii.

[7] Picha hii ya vipindi vya mwaka imetolewa hapa: http://www.google.de/imgres?imgurl=http://thankevann.com/hsg/images/lit_cycle.gif&imgrefurl=http://thankevann.com/homeschoolgoodies/%3Fpage_id%3D48&h=328&w=330&sz=27&tbnid=043npo9z3ftnoM:&tbnh=118&tbnw=119&prev=/images%3Fq%3Dimage%2Bliturgical%2Byear&hl=de&usg=__M9ru-kB9Nmnd3j2mMZjKZP0WoAk=&sa=X&ei=spQ1TJijI4SsOPWR0asE&ved=0CDMQ9QEwBg

Share this post
Repost0
To be informed of the latest articles, subscribe:
Comment on this post
H
Wonderful learning guys I’m a fan of your website.
Reply
L
upport you and wish you a good continuation.
Reply
S
Really the blogging is spreading its wings rapidly. Your write up is a fine example of it.
Reply
R
discount swarovski crystal jewelry , rainbow crystal , swarovski.co.uk , swarovski maskerade ,
Reply
T
I dead consider joyous when I acquire articles pertinent to my process and my issue.
Reply