Overblog
Edit post Follow this blog Administration + Create my blog
liturjia-takatifu.over-blog.com's name

Hii blog ni kwa ajili ya kuitikia mwaliko wa Mtaguso wa pili wa Vatikano wa kuwafanya wakatoliki wote waifahamu liturjia takatifu wanayoiadhimisha. Nitatoa utafiti wangu juu ya liturjia na nitakuwa tayari kujibu maswali yenu juu ya liturjia. Karibuni sana!The aim of this blog is to impart liturgical knowledge to the people of God. It targets mainly the people from the swahili speaking countries. Welcome for the sharing of knowledge about our liturgy!

Sherehe ya Bwana wetu Yesu Kristu Mfalme

Sherehe ya Bwana wetu Yesu Kristu Mfalme

Jumapili ya 34 ya Mwaka

 

king.jpgKesho tunaadhimisha sherehe ya Bwana wetu Yesu Kristu Mfalme. Sherehe hii uangukia Jumapili ya mwisho ya mwaka wa Kanisa, yaani Jumapili ya 34 ya mwaka. Baada ya juma tunalolianza kesho tutaanza kipindi cha majilio. Tutakuwa pia tumeanza mwaka mpya wa Kanisa. Kwa ufupi tu tuzungumzie juu ya Sherehe yetu ya kesho.

Sherehe ya Kristu Mfalme iliwekwa rasmi na Papa Pio XI mwaka 1925. Papa Pio XI alifanya kila Jumapili  kabla ya Sherehe wa Watakatifu wote  ya tarehe 1 Novemba (Jumapili ya mwisho wa mwezi Oktoba) kuwa Jumapili ya Kristu Mfalme. Sio kwamba Kanisa lilikaa mpaka mwaka huo wa 1925 bila kuadhimisha ufalme wa Kristu. Ufalme wa Kristu unaadhimishwa pia katika sherehe za Epifania, Pasaka  na Kupaa mbinguni kwa Bwana wetu Yesu Kristu. Nia maalum ya Baba Mtakatifu Pio XI iliwekwa wazi katika waraka wa kipapa ujulikanao kama Quas primas (11 Desemba 1925).  Baba Mtakatifu huyo alitaka sherehe hiyo iwe nyenzo ya kuboresha maisha ya kiroho ya watu ambao kwa wakati huo yalihatarishwa na kusambaha kwa nguvu za giza kama kutomwamini Mungu na mambo mengine ya kidunia ya wakati huo. Baba Mtakatifu alitaka kutuhakikishia ufalme, utawala na uweza wa Kristu katika maisha yetu na jumuiya. Tunamhitaji Kristu katika maisha yetu awe mtawala na kiongozi. Hata sasa kwa hali tuliyonayo watu wanatawaliwa mambo mabaya kwa hiyo ni muhimu kukumbuka kuwa Kristu ni mfalme na mtawala wa maisha yetu na serikali zetu.

Katika Misale ya Kirumi iliyotolewa baada ya mtaguso wa pili wa Vatikano ya mwaka 1970, sherehe hii iliwekwa Jumapili ya mwisho ya Mwaka, yaani Jumapili ya 34 ya mwaka. Nafasi hii inatuonyesha wazi kuwa Kristu ni mfalme wa Ulimwengu wote na nyakati zote. Katika Misale hii sherehe inabeba uzito wa kutukumbusha kuja kwake Kristu mara ya pili katika utukufu kama mtawala wa mbingu na nchi. Inatuashiria mambo ya mwisho wa dunia na nyakati zijazo. Mada hii ya kurudi kwake Kristu katika utukufu inapatikana katika sala ya mwanzo ya kesho isemayo: “Ee Mungu Mwenyezi wa milele, umependa kutengeneza upya mambo yote katika Mwanao mpenzi, Mfalme wa ulimwengu. Utujalie kwa wema wako, viumbe vyote vilivyokombolewa utumwani vikutumimie na kukusifu bila mwisho. Tunaomba hayo kwa njia ya Bwana...”[1]

 

Nawatakia Sherehe njema ya Kristu Mfalme na Baraka za Mwenyezi Mungu!!!

G. Mutarubukwa

 

Vyanzo:

Misale ya Waumini, T.M.P Book Department, Tabora 91974.

Sala ya Kanisa, Benedictine Publications, Ndanda-Peramiho 31983.

Adam A., The Liturgical Year: Its History & Its Meaning after the Reform of the Liturgy, New York 1981, 177-180.

Augé M., Anno Liturgico: Storia, Celebrazione, Teologia, Spiritualità, Roma 2006.

Jounel P., “The Year”, The Liturgy and Time, The Church at Prayer 4, ed. A. G. Martimort, Collegeville1986, 106-107.[1] Misale ya Waumini, T.M.P Book Department, Tabora 91974, 774.

 

NB: Picha ya Kristu Mfalme imetolewa hapa: http://www.therealpresence.org/eucharst/link/e-jesus.html

Share this post
Repost0
To be informed of the latest articles, subscribe:
Comment on this post
E
Yesu wetu
Reply
E
Yesu wetu
Reply
G
<br /> Nashukuru sana Fr. kwa kutufunza na kutlisha neno la Mungu kwa njia hii. Nakuombea ili usipotee kwa kipindi kirefu maana mimi nimfatiliaji mzuri wa hii blog. Nakutakia utume mwema.<br /> <br /> <br />
Reply