Overblog
Edit page Follow this blog Administration + Create my blog
liturjia-takatifu.over-blog.com's name

Hii blog ni kwa ajili ya kuitikia mwaliko wa Mtaguso wa pili wa Vatikano wa kuwafanya wakatoliki wote waifahamu liturjia takatifu wanayoiadhimisha. Nitatoa utafiti wangu juu ya liturjia na nitakuwa tayari kujibu maswali yenu juu ya liturjia. Karibuni sana!The aim of this blog is to impart liturgical knowledge to the people of God. It targets mainly the people from the swahili speaking countries. Welcome for the sharing of knowledge about our liturgy!

Ijumaa Juma la 21 Mwaka A (26 Agosti 2011)

Masomo ya Misa 

Ijumaa Juma la 21 Mwaka A

MWAKA 1, Somo 1                                                     1 The. 4: 1-8

Mashauri juu ya kuishi kitakatifu.

Somo katika waraka wa kwanza wa Mtume Paulo kwa Wathesalonike.

Ndugu, tunakusihini na kuwaonya kwamba mwenende katika Bwana Yesu; kama mlivyopokea kwetu jinsi iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kama nanyi mnavyoenenda, vivyo hivyo mpate kuzidi sana. Kwa kuwa mnajua ni maagizo gani tuliyowapa kwa Bwana Yesu.

Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu. Mtu asimpunje ndugu yake wala kumkosa katika jambo hili; kwa sababu Bwana ndiye alipizaye kisasi cha haya yote; kama tulivyowaambia kwanza, tukashuhudia sana. Maana Mungu hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso. Basi yeye anayekataa, hakatai mwanadamu bali Mungu, anayewapa ninyi Roho wake Mtakatifu.

Hilo ndilo neno la Mungu.

 

Wimbo wa Katikati:                     Zaburi  97: 1-2, 5-6, 10-12 (K) 12

1.   Bwana ametamalaki, nchi na ishangilie,

visiwa vingi na vifurahi.

Mawingu na giza vyamzunguka

Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chake

 

(K) Enyi wenye haki, mfurahini Bwana.

 

2.   Milima iliyeyuka kama nta mbele za Bwana,

Mbele za Bwana wa dunia yote.

Mbingu zimetangaza haki yake,

na watu wote wameuona utukufu wake. (K)

 

3.   Enyi mmpendao Bwana, uchukieni uovu;

Huwalinda nafsi zao watauwa wake,

na kuwaokoa  na mkono wa wasio haki. (K)

 

4.   Nuru imemzukia mwenye haki,

na furaha wanyofu wa moyo.

Enyi wenye haki, mfurahieni Bwana,

Na kulishukuru jina lake takatifu. (K)

 

Shangilio:                                                                           Yn.  15: 15

Aleluya, aleluya,

Bwana anasema: Siwaiti tena watumwa,

lakini ninyi nimewaita rafiki,

kwa kuwa yote niliyoyasikia

kwa Baba yangu nimewaarifu.

Aleluya.


MWAKA 1 NA 2, INJILI                                                      Mt 25:1-13

Kesheni kwani hamjui siku wala saa. Mfano wa wanawali kumi.

Somo katika Injili ilivyoandikwa na Mathayo.

Yesu aliwaambia wafuasi wake: Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi. Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara. Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao; bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao. Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi.

Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki. Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao. Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika. Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo; hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie. Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, ano waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa.

Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie. Akajibu akasema, Amin, nawaambia, siwajui ninyi. Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa.

Hilo ndilo neno la Mungu

 

Kutoka: Masomo ya Misa, T.M.P Book Department, Tabora 1975 (Swahili Lectionary) 

 

Share this blog
Repost0
To be informed of the latest articles, subscribe: