July 31 2010
Kesho tarehe 1 Agosti 2010 katika Kanisa la Parokia ya Mt. Petro mjini Wolfenbuettel, Ujerumani, kutakuwa na adhimisho maalum la Ekaristi Takatifu lijulikanalo kama "Afrikanische Messe" yaani Misa ya kiafrika. Itakuwa kesho saa 5 asubuhi na kuendelea. Hii kwangu ni mara ya tatu kuwa na adhimisho kama hili hapa. Baada ya Misa tunakuwa na mlo wa pamoja na baadaye kila mtu anaondoka kwa wakati wake.
Kesho mada kuu itakuwa juu ya Jumuiya Ndogo ndogo za Kikristu na maisha ya Kikristu. Hapa pia wana mawazo ya kuanzisha Jumuiya za namna hiyo ili kusaidia katika uimarishaji wa imani na uinjilishaji.
Basi usikose habari nitakayokuletea baada ya tukio hilo la kesho, ili uweze kujua nini kinafanya Misa hiyo iitwe ya kiafrika au ipewe kivumishi katika lugha ya Kijerumani "Afrikanische".
G. Mutarubukwa